Na Carlos Claudio Dar es Salaam.📍
Wananchi wameendelea kuingia kwa wingi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara maarufu Sabasaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Julai 7, 2026.
Hali ya usalama imeendelea kuwa shwari huku waandaaji na vyombo vya ulinzi wakihakikisha wageni wanapata huduma katika mazingira salama na yenye utulivu.
Tags
HABARI KITAIFA
