TTCL YAONESHA SULUHUISHO ZA KIDIJITALI SABASABA 2026

 


Na Carlos Claudio, Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Telecommunications Corporation, Moremi Marwa, ametembelea banda la shirika hilo katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2026 na kuwakaribisha wananchi kujionea huduma na suluhisho mbalimbali za kidijitali zinazotolewa na TTCL.


Marwa amesema ushiriki wa TTCL katika maonesho hayo unalenga kuendelea kuwasogezea wananchi teknolojia za kisasa zinazorahisisha mawasiliano, biashara na upatikanaji wa huduma mbalimbali za kidijitali.



Amesema kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, huduma za Faiba, FTTX Experience Centre, Cloud Computing kupitia Kituo cha Taifa cha Data (NIDC), pamoja na suluhisho nyingine za kisasa, TTCL inaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini.


Kwa mujibu wa Marwa, huduma hizo zina mchango mkubwa katika kuwaunganisha Watanzania, kukuza biashara za kidijitali na kuwezesha taasisi za umma na binafsi kutumia teknolojia kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.


Ameongeza kuwa TTCL itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya mawasiliano na teknolojia ili kuhakikisha wananchi, wafanyabiashara na taasisi wanapata huduma bora, salama na za uhakika.


Aidha, amewaalika wananchi kutembelea banda la TTCL katika Maonesho ya Sabasaba 2026 ili kujionea teknolojia mbalimbali zinazobadilisha maisha ya kila siku na kufungua fursa mpya za biashara katika uchumi wa kidijitali.


🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA

Previous Post Next Post