WELLWORTH COLLECTION YAHAMASISHA UTALII WA NDANI, YAJIPANGA KWA AFCON 2027


Na Carlos Claudio, Dar es Salaam.📍


Kampuni ya huduma za malazi na utalii ya Wellworth Collection imetumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, maarufu Sabasaba, kuhamasisha utalii wa ndani huku ikiendelea kupanua uwekezaji wake kuelekea fursa zinazotarajiwa kujitokeza wakati wa mashindano ya AFCON 2027.


Akizungumza katika banda la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ofisa Mauzo wa Wellworth Collection, Sharmila Omari, amesema kampuni hiyo inawaalika Watanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii kupitia hoteli, lodge na kambi zake zilizopo katika maeneo tofauti nchini.


Amesema kampuni hiyo kwa sasa inasimamia lodge tano za nyota tano, kambi nne za kifahari pamoja na resort mbili, ikiwemo moja iliyopo Zanzibar, huku resort nyingine ikiendelea kukamilishwa jijini Dar es Salaam.



Kwa mujibu wa Sharmila, kampuni hiyo pia inaendelea kuitangaza Mikumi kama moja ya maeneo yenye fursa kubwa kwa watalii wa ndani, akieleza kuwa maboresho ya miundombinu ya usafiri, ikiwemo huduma za Standard Gauge Railway (SGR), yanarahisisha safari za watalii kuelekea maeneo mbalimbali ya utalii.


Katika maonesho hayo, Wellworth Collection inatoa ofa maalum za malazi kuanzia Sh762,000 kwa watu wawili, zikiwa zinajumuisha huduma za chakula.


Sharmila amesema kampuni hiyo pia inamiliki Kunduchi Wet 'N' Wild na imeendelea kuandaa vifurushi vinavyounganisha utalii wa hifadhi za wanyamapori na mapumziko ya fukwe za bahari.



Ameongeza kuwa Wellworth Collection inaendelea kujenga lodge na kambi mpya katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ili kuongeza uwezo wa kupokea wageni wanaotarajiwa kuwasili wakati wa AFCON 2027.


“Tunajiandaa kupokea wageni wengi zaidi kuelekea AFCON 2027. Tunawahimiza Watanzania na wageni kufanya nafasi mapema ili kunufaika na ofa zilizopo,” amesema Sharmila.



🚨Full Video Inapatikana Katika YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post