Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.📍
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetoa wito kwa wananchi kutambua kuwa kudai haki zao kunapaswa kwenda sambamba na kutekeleza wajibu wao kwa kuheshimu sheria, kulinda haki za wengine na kushiriki katika kujenga jamii inayozingatia misingi ya haki na utawala bora.
Wito huo umetolewa na Afisa Uchunguzi Mkuu wa tume hiyo, Bi. Happy Mtei, wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la Tume katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Dar es Salaam leo Julai 06, 2026.
Bi. Mtei alisema pamoja na wananchi wengi kufahamu haki zao za msingi, bado kuna haja ya kuendelea kutoa elimu kuhusu wajibu unaoambatana na haki hizo ili kupunguza migogoro na kuimarisha mshikamano wa kijamii.
"Kila mwananchi anatakiwa kutambua kuwa haki huambatana na wajibu. Huwezi kudai haki zako huku ukikiuka haki za wengine. Tunapaswa kuheshimu sheria, kutimiza wajibu wetu na kutumia njia zinazotambuliwa na sheria tunapotafuta haki," amesema Bi. Mtei.
THBUB imeendelea kutumia Maonesho ya Sabasaba kama jukwaa la kutoa elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na utawala bora, kupokea malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu na kutoa ushauri wa masuala ya hali za binadmau na utawala bora.
🚨Suscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.







