SERIKALI YASHAURIWA KUSHUGHULIKIA KERO ZINAZOWATESA WATANZANIA.


Na Mwandishi wetu,Dodoma.📍


ASKOFU wa Kamisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika  Dk, Dickson Chilongani,amehitaka Serikali ya Tanzania kushughulikia kero zinazowasumbua watanzania ili watu wawe na amani ikiwa ni pamoja na kutenda haki.


Ametoa kauli hiyo leo katika Ibada ya siku ya sherehe ya kumbukizi ya kufufuka Yesu Kristo iliyofanyika katika kanisa kuu la Roho Mtakatifu lililopo Jijini Dodoma.


Katika sherehe ya kumbukizi hiyo ambayo ufanywa na wakristo wote ulimwenguni Asofu Dk.Chilongani amesema kuwa serikali iongeze jitihada za kushughulikia kero mbalimbali ili watanzania wawe na furaha. 


"Tunashukuru mwaka jana mishahara iliongezwa lakini bado kuna kero nyingi kwenye maofisi."ameeleza askofu Dk.Chilongani.


Kiongozi huyo wa Kiroho amesema kuwa bado kuna  kero za ukilitimba, kero za kunyimwa haki na kero za rushwa. 


Amesema kuwa kwa sasa ofisi nyingi zinafanya vitendo vya kuomba rushwa kwa kutumia msemo wa kudai uwezwshwaji “facilitation” na mambo hayo yanafanyika wazi wazi na rushwa zinaombwa wazi wazi. 


"Unamtuma mfanyakazi ashughulikie suala muhimu anakwambia Baba Askofu tukienda wanatuomba facilitation. 


"Hawaoni aibu hata kuliomba Kanisa litoe facilitation,tuiombe Serikali itupie macho kero hizi ili Watanzania waishi kwa furaha"ameeleza Chilongani.


Katika kuitimisha mahubiri yake Askofu Dk.Chilongani amesema kuwa tunashukuru kwa amani ambayo inaendelea, umoja na mshikamano wa Watanzania.


"Naomba niongeze kwamba kama malaika alivyowafanya wamama wale wasahau changamoto za kulivingirisha jiwe wakawa na furaha, na Serikali inatakiwa kuhakikisha watanzania wanakuwa na furaha,amani mshikamano kwa kuondoa kero ambazo ni kero kwa watanzania"amehitimisha askofu Dk.Chilongani.

🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post