MBEYA, TANZANIA📍 – 05 APRIL, 2026
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo amewajumuika na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka. Ibada hiyo imefanyika katika Usharika wa Lawi, uliopo Jimbo la Mbeya Mashariki, Dayosisi ya Konde.
Chatanda ameshiriki ibada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuungana na Watanzania katika kuadhimisha ufufuo wa Yesu Kristo, tukio ambalo ni msingi wa imani ya Kikristo duniani kote.
Katika salamu zake, Chatanda amewasihi waumini na Watanzania wote kuendelea Kuliombea Taifa letu amani na utulivu pia Kumuombea Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili Mwenyezi Mungu azidi kumpa hekima na nguvu ya kuliongoza Taifa letu kwa mafanikio makubwa.


