Na Barnabas Kisengi , Dodoma .📍
Maafisa Usafirishaji Bodaboda wa mtaa wa chinyoyo kata ya kilimani wameaswa kuhakikisha wanakwenda shule ili waweze kusoma na kujipatia vyeti na leseni kwa kozi za muda mfupi.
Kauli hiyo umetolewa mapema leo February 23 2026 na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe Paskali Chinyele alipokuwa akizungumza na maafisa Usafirishaji hao katika kijiwe cha sheli mbili chinyoyo.
"Niwaambie vijana wangu jitahidini kuona umuhimu wa kusomea udereva ili mpate cheti na leseni zenu tambueni kuwa nyingi ni watu muhimu sana katika swala la Usafirishaji wa abiria Sasa msijione kuwa wanyonge jitahidini kuhakikisha mnakwenda shule"amesisitiza Mhe Chinyele
"Kwakuwa kazi yenu ni ajira rasmi mnatambulika kama maafisa Usafirishaji Sasa hapa kikubwa ni kuhakikisha mnakuwa na uongozi wenu na wale wote ambao hawana vyeti wala leseni mnajiorodhesha kwa viongozi wenu ili nipate idadi yenu kupitia kwa Diwani wenu au Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huu ili tuweze kuwaunganisha muweze kupatiwa mafunzo ya muda mfupi na mpatiwe vyeti na leseni zenu halali"amesema Mhe Chinyele
Aidha Mbunge Chinyele amesema fursa za pikipiki za mikopo zipo nyingi ila vigezo vingi vinawashindwa kwa kukosa vyeti na leseni hivyo amewataka vijana wao kwanza kuweka kipaombele cha kupata elimu ili wawe na vyeti na leseni ambavyo vitawasaidia sana.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya kilimani Mhe Mussa Mkunda amewataka maafisa Usafirishaji Bodaboda hao kusajili vijiwe vyote vya mtaa huo na kuwa na orodha kamili ya majina ya Bodaboda wa kila kijiwe katika Mtaa huo.
"Niwaambie vijana hakikisheni wote mmesajili vijiwe vyenu na kuwa na namba pia kuhakikisha katika vijiwe vyenu vyote mnakuwa na orodha kamili ya majina na mnatambuana katika maeneo yenu"amesisitiza Mhe Diwani Mkunda
Diwani Mussa Mkunda amesema kuwa kutokana na kutambulika kama maafisa Usafirishaji Bodaboda kuna fursa ya mikopo ya vijana katika halmashauri ya Jiji la Dodoma hivyo amewataka vijana kujiunga katika vikundi ili waweze kunitumia fursa hiyo ya mikopo ya kundi la vijana ili waweze kujiinua kiuchumi kama kikundi na mtu moja moja.
Kwa upande wao maafisa Usafirishaji Bodaboda wa mtaa wa chinyoyo wamesema maelekezo hayo waliyopewa na viongozi wao Mbunge na Diwani wameyapikea na watayafanyia kazi kwa haraka.
Awali akiwapokea viongozi hao Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM tawi la chinyoyo Comredi Casto Muhilu amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakiendesha Bodaboda lakini wakiwa hawana vyeti wala leseni pia changamoto nyingine waliomba kujengewa mabanda katika vijiwe vyao ili katika kipindi cha mvua na juwa wawe katika mazingira salama kwa kuwasubiri wateja wao.





