SCANCODE TANZANIA YAIPONGEZA UMO KWA KUANDAA MATENDO YA HURUMA DODOMA

 


Na Bakari Kiwingu, Dodoma📍


Uongozi wa Scancode Tanzania waipongeza taasisi ya uchumi na maendeleo organization (UMO) kwa kuwakutanisha wadau katika kufanikisha matukio ya matendo ya huruma yaliyoandaliwa na taasisi hiyo ya umo kwa kwenda kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Rahman kilichopo Chang'ombe kata ya Chang'ombe  dodoma mjini  jana February 20,2026.


Akitoa salamu shukrani na pongezi  kwa niaba ya mkurugenzi wa Scancode Tz. Balozi wa Scancode Bakari Kiwingu amesema matendo yaliyofanywa na taasisi ya umo ni jambo la kuigwa katika jamiii kwani kufanya ni jambo jema ambalo linaleta faraja,amani na upendo kwa watoto  wanaishi kwenye vituo vya kulelea watoto yatima na wenye mahitaji maalum nchini hivyo serikali na taasisi zisizo za kiserikali na wadau mbalimbali wanapaswa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi ya umo ili iweze kufanikisha malengo waliojiwekea katika kuitumikia jamii kwa maslahi mapana ya taasisi yao na Taifa.



Aidha Balozi kiwingu ametoa wito kwa jamii kujitafakari kufuatia mfungo huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma kwa kutubu na  kutendo mema yatakayompendeza na kumfurahisha Mungu ikiwe kuwasaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalum kwa kile wachojaaliwa na Mungu hii itaongeza upendo na thamani mbele ya jamii 


Katika hatua nyengine balozi kiwingu amewaomba watanzania wote nchini kuendelea kudumisha amani na kuwaombea viongozi afya njema ili waweze kulitumikia vyema Taifa 





Story by.bk

🚨Full Video Inapatikana Katika YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA

Previous Post Next Post