Na Carlos Claudio, Dodoma.📍
Tamasha maalum lenye lengo la kuwaelimisha vijana kuhusu kuishi maisha ya maadili kupitia muziki wa injili linatarajiwa kuangazia jiji la Dodoma Disemba 13, 2025. Tamasha hilo, linaloitwa Usiku wa Sifa 2025, limeandaliwa na Kwaya ya Uvuke ya Uinjilisti kutoka Kanisa Kuu la Anglikana Dodoma.
“Tunatumia muziki kuwafikia vijana kwa sababu injili ina mafundisho mengi kuhusu maadili, upendo na uwajibikaji,” amesema Kuchaka.
Tamasha hilo linatarajiwa kuwavuta zaidi ya watu 1,000 na litakuwa moja ya matukio makubwa ya injili mkoani Dodoma mwaka huu. Kwaya na waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa watapamba jukwaa kupitia uimbaji, kusifu na kuabudu.
Miongoni mwa kwaya zitakazoshiriki ni VVC Choir kutoka Dar es Salaam, SRC Choir kutoka Arusha, na Neema Gospel kutoka Dar es Salaam kama wageni maalum. Kutoka Dodoma watakuwepo wenyeji Kwaya ya Uvuke, Safina Anglican Choir, na The Winners Group wa Dodoma.
Burudani hiyo ya kiroho itaongozwa na MC Madevu kutoka Dar es Salaam, ambaye anatarajiwa kuongeza mvuto na ubora wa usiku huo. Pia mchekeshaji maarufu nchini, Eliud Samuel, atapamba tukio hilo kwa ucheshi wa kiimani utakaolenga kuleta tabasamu kwa waumini na wageni wote.
Kwa upande wa viingilio, maandalizi yamegawanywa katika madaraja tofauti.
- Special Seats: Shilingi 100,000 kwa kila kiti, ikijumuisha chakula, vinywaji na sofa la hadhi.
- Meza Maalum (Watu 5): Shilingi 500,000 ikiwemo chakula, vinywaji na huduma zote za mezani.
- VVIP: Shilingi 50,000, watapata bites, vinywaji baridi na siti maalum.
- VIP: Shilingi 30,000, wakipatiwa vinywaji baridi na siti yenye mapambo maalum.
- Kawaida: Shilingi 10,000 kwa huduma za ibada na burudani.
Waandaaji wametoa mwaliko kwa wadhamini, taasisi, kampuni na wadau mbalimbali kuunga mkono tamasha hilo ili kuendeleza kazi ya injili, kukuza vipaji na kuimarisha mshikamano wa kiroho.
Makusanyo yanayotarajiwa yatasaidia kuanzisha miradi ya maendeleo kwa ajili ya kuendeleza huduma na kusaidia jamii yenye uhitaji.
Kwa mawasiliano na ushiriki, watahitaji kufika au kupiga simu kupitia namba 0626 758 470 au 0785 105 353.
Tamasha la Usiku wa Sifa 2025 linatarajiwa kuwa usiku wa ibada, ushuhuda, shukrani na burudani ya kiimani ya kiwango cha juu kwa wakazi wa Dodoma na wageni kutoka maeneo mbalimbali nchini.
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.







