MAVUNDE AANZISHA UJENZI WA ZAHANATI MASEYA–HOMBOLO MAKULU



Na Mwandishi wetu, Dodoma📍.


Mbunge wa Jimbo la Mtumba, Anthony Mavunde, amezindua rasmi ujenzi wa zahanati katika Mtaa wa Maseya, Kata ya Hombolo Makulu, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 Uzinduzi huo uliohudhuriwa  na wananchi wa kata ya hambo ambao wamesema hatua hiyo inaleta matumaini ya kusogeza huduma za afya karibu na jamii.


Katika uzinduzi huo, Mavunde ameahidi kushiriki kikamilifu kukamilisha ujenzi huo kwa wakati, huku akichangia matofali 2,000 na mifuko 100 ya saruji ili kuhakikisha jengo linakamilika hadi hatua ya upasuaji, Amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni kielelezo cha uwajibikaji wa viongozi na matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wananchi na serikali.


Kwaupande wao Wananchi, Mwenyekiti wa Mtaa wa Maseya Alexander Fwalu  wamesema hatua hiyo itaokoa muda na gharama walizokuwa wakitumia kufuata huduma za afya maeneo ya mbali huku wakieleza utayari wao wa kushiriki kikamilifu katika kazi za ujenzi ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.








🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post