HECHE AITAKA MAHAKAMA KESI YA LISSU KURUDI HARAKA KUSIKILIZWA

 


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM.📍


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, JOHN WEGESA HECHE, ameomba Mahakama Kuu ya Tanzania kuhakikisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, TUNDU LISSU, inarudi haraka kusikilizwa ili iweze kufikia tamati.


Akizungumza leo, Novemba 12, 2025, nje ya viunga vya Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, HECHE alisema ni siku 225 zimepita tangu Mwenyekiti wao awe kizuizini, hali ambayo amesema inaleta mashaka juu ya utolewaji wa haki kwa wakati. Alisisitiza kuwa ni muhimu kesi hiyo kuendelea bila ucheleweshaji ili wananchi wapate kuona haki ikitendeka.


Kesi hiyo ya uhaini imeahirishwa hadi Msajili wa Mahakama atakapopanga ratiba mpya, kutokana na kusikilizwa kwa mfumo wa vipindi (sessions). HECHE pia alitangaza kuwa CHADEMA imewateua mawakili nchi nzima kuwawakilisha wanachama na wananchi wote wanaokabiliwa na mashtaka ya uhaini, akisema chama hicho kitasimama bega kwa bega na wote wanaodai haki na demokrasia nchini.



🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post