BABA LEVO AAPA KUWAKILISHA WANANCHI WA KIGOMA MJINI BUNGE LA 13.

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.📍


Mbunge mpya wa Kigoma Mjini, Revocatus Chipando, maarufu kama Baba Levo au Kibarabara, ameapishwa rasmi leo Novemba 11, 2025, Jijini Dodoma, kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo hilo katika Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Hafla ya kuapishwa kwake imefanyika mbele ya Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, ambapo Baba Levo ameahidi kulitumikia jimbo lake kwa uadilifu, ubunifu na uwazi.


Akizungumza baada ya kuapishwa, Chipando amesema atatumia nafasi hiyo kuimarisha maendeleo ya vijana, kukuza uchumi wa wananchi wa Kigoma na kuhimiza matumizi ya fursa za kijamii na kiuchumi.


Wananchi wa Kigoma Mjini wamepokea habari hizo kwa furaha, wakimpongeza kwa hatua hiyo na kumtaka atumie umaarufu wake katika sanaa kuibua na kushughulikia changamoto za wananchi.




🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post