MAVUNDE: MILIONI 204 KUJENGA MADARASA MAPYA SHULE YA WEYULA.

 


Dodoma.📍

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtumba, Anthony Mavunde, amesema Shule ya Msingi Weyula itajengewa madarasa mapya 8 kwa ufadhili wa shilingi milioni 204 kutoka kwa wadau wa maendeleo, nje ya bajeti ya serikali.


Amesema lengo la ujenzi huo ni kupunguza msongamano wa wanafunzi na kuboresha mazingira ya kujifunzia, akibainisha kuwa shule hiyo ni ya zamani na madarasa yaliyopo kwa sasa yamechakaa, hivyo kuhitaji maboresho ya haraka.


Mavunde amesema fedha hizo ni matokeo ya jitihada zake za kutafuta rasilimali za maendeleo ya elimu, na kwamba pia anapanga kununua mitambo ya kudurufu mitihani ili kuwapunguzia mzigo wazazi.



Akiwa katika kampeni Kata ya Makutupora, amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa sekta ya ardhi, zikiwemo upimaji na urasimishaji wa maeneo, huku akiahidi kila mwananchi kumilikishwa ardhi kupitia utaratibu rasmi.


Aidha, ametangaza mpango wa kuanzisha klabu za wazee kila kata kwa ajili ya kuboresha afya zao kupitia michezo na shughuli za kijamii, sambamba na kuanzisha taasisi kwa ajili ya kusaidia watoto yatima na wazee wasiojiweza.


Katika sekta ya michezo, Mavunde ameahidi kugawa jezi na mipira kwenye mitaa yote ya jimbo hilo ili kukuza vipaji na mshikamano wa vijana.










🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post