Dodoma.📍
Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtumba, Anthony Mavunde, ameendelea na kampeni zake katika Kata ya Miyuji, ambapo ameahidi kuwaletea wananchi madaktari bingwa kwa ajili ya kliniki ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ili kuwapima na kuwatibu bure.
Mavunde amesema hatua hiyo inalenga kuboresha afya za wakazi wa Dodoma, hasa wale wasio na uwezo wa kugharamia matibabu ya kitaalamu.
"Wananchi wa Dodoma mnafahamu, nitaleta madaktari bingwa kuwapima na kuwatibia bure," amesema Mavunde.
Aidha, amewahakikishia vijana wa bodaboda kuwa safari hii watapata pikipiki zao wenyewe, kama sehemu ya juhudi za kuwawezesha kiuchumi.
Pia, Mavunde amegusia changamoto ya ubovu wa daladala, hususan eneo la Maili Mbili kwa Mohammed, akiahidi kuwa wananchi wa jimbo hilo watanunua greda lao wenyewe kwa ajili ya kutengeneza barabara katika kata zote 20 za Jimbo la Mtumba.
Vilevile, ameeleza kuwa tayari amezungumza na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) kuhusu mpango wa kuanzisha mzunguko wa daladala zitakazotoa huduma kutoka mjini kwenda Miyuji, ili kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi.
Mavunde amesisitiza kuwa malengo yake ni kuhakikisha wananchi wa Mtumba wanapata maendeleo yanayoonekana kupitia huduma bora za afya, elimu, miundombinu na ajira kwa vijana, wanawake na makundi maalum.
🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.


