MAVUNDE AAHIDI FIDIA, HUDUMA BORA NA HATI MILIKI KWA WANANCHI WA MTUMBA



Dodoma.📍

Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Peter Mavunde, ameendelea kuwawasilisha dira yake ya maendeleo inayolenga kuibadilisha Mtumba kuwa kitovu cha ustawi wa kijamii na kiuchumi.


Akizungumza na wananchi wa kata ya Msalato kwenye muendelezo wa Kampeni zake Mavunde amebainisha maeneo kadhaa ya kipaumbele, ikiwemo kuhakikisha fidia stahiki inatolewa kwa wananchi waliopitiwa na miundombinu ya umeme, ili kulinda haki zao na kuondoa changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya kitaifa.


Aidha, ameahidi kusogeza huduma za kijamii kama afya, elimu, maji na miundombinu bora katika kila mtaa, akisisitiza kwamba maendeleo ya kweli yanapaswa kumgusa kila mwananchi bila kujali eneo analoishi.



Wakati huo huo, katika Mtaa wa Chikole, Mavunde ametangaza mpango wa kuchimba visima viwili vipya katika shule ya msingi na sekondari za mtaa huo ili kuboresha upatikanaji wa maji safi kwa wanafunzi na jamii inayowazunguka.


Katika kuhakikisha usalama wa umiliki wa ardhi, Mavunde amesema atahakikisha wananchi wote wanapatiwa hati miliki za ardhi kwa mujibu wa sheria, hatua itakayoongeza thamani ya mali zao na kuleta utulivu wa kimaendeleo.


Akihitimisha mkutano huo, amesisitiza umuhimu wa kujenga mahusiano mazuri kati ya wananchi na mamlaka za serikali, sambamba na kulinda haki na maslahi ya wananchi wote kwa misingi ya uwajibikaji, ushirikiano na uwazi.




🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post