MAVUNDE AAHIDI KUKAMILIKA KWA KIWANGO CHA LAMI BARABARA YA NZUGUNI-MAHOMANYIKA.

Dodoma.📍

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtumba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde, ameahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa anazifahamu kwa undani na zipo moyoni mwake.


Amesema moja ya vipaumbele vyake ni kusimamia Ilani ya Uchaguzi ya CCM juu ya ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara ya kilomita 7 kutoka Nzuguni mwisho wa lami mpaka Mahomanyika sambamba na kufungua barabara za mitaa ili kuhakikisha zinapitika wakati wote ili kupunguza gharama za usafiri kwa wananchi, huku akiweka  mpango wa kununua greda la jimbo la Mtumba litakalotumika kusafisha na kufungua barabara za kata na mitaa mbalimbali.


Katika sekta ya kilimo, Mavunde amesema atachimba kisima katika eneo la Mbugani Mahoma Nyika ili kuwezesha vijana kufanya kilimo cha umwagiliaji chenye tija na kuongeza ajira.


Ameeleza pia dhamira yake ya kukamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Kitelela, ambayo itasajiliwa rasmi na kufanya mitihani katika eneo hilo hilo, sambamba na kuanzisha ujenzi wa Shule ya Sekondari Mahoma Nyika.


Kwa upande wa elimu ya msingi, amepanga kujenga madarasa na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Mahoma Nyika ili kuboresha mazingira ya kujifunzia.


Aidha, Mavunde ameahidi kuanzisha ujenzi wa zahanati katika Kata ya Nzuguni, akisema yuko tayari kushirikiana na serikali kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa mafanikio.



🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post