VIONGOZI WA CCM WAIOMBA HAZINA KUMCHAGUA KAYOMBO

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Mgombea udiwani kata ya Hazina kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Lukanus Kayombo, ameahidi kuendeleza jitihada za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi mara atakapopewa ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo.


Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, Kayombo alisema uzoefu wake wa zaidi ya miongo mitatu akiwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kinyagwaroad, pamoja na utumishi wa zaidi ya miaka 30 serikalini, unampa ujasiri wa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Hazina kwa uadilifu na vitendo.



Kazi yangu mnaifahamu. Nikiwa mwenyekiti nimejenga ofisi ya serikali ya mtaa, nimewapatia wazee bima ya afya. Sasa mmeniongezea daraja, nawahakikishia hili daraja tutalifanya pamoja kwa maendeleo ya Hazina,” alisema Kayombo.


Katika uzinduzi huo, mgombea wa udiwani kata ya Ipagala, Mhe. Gombo Kamuli Dotto, alimuwakilisha Katibu wa CCM Dodoma Mjini, Samuel Ikwabe, na kuwasihi wananchi wa kata ya Hazina kumpa kura Kayombo ili kuunda Halmashauri imara ya Jiji la Dodoma itakayojikita katika kuwaletea wananchi maendeleo.


Aidha, Mhe. Gombo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. 

Samia Suluhu Hassan, akibainisha mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya Jiji la Dodoma ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), barabara ya pete (ring road) na uwepo wa makao makuu ya serikali.


Wana Dodoma sasa tunajivunia SGR, barabara ya mzunguko na miradi mikubwa ya uwekezaji. Hakuna mkoa mwingine Tanzania uliyopewa barabara ya pete na ikakamilika kama Dodoma. Haya yote ni kazi ya Rais Samia, hivyo naomba kura zenu za ndiyo kwake, alisema.


Kwa upande mwingine, aliwatambulisha wagombea wengine wa CCM akiwemo Pascal Chinyele, akimtaja kama kiongozi mwenye msimamo thabiti na uwezo wa kufuatilia maendeleo ya wananchi, akisisitiza kuwa atakuwa ziada ya Mavunde kwa mbele kidogo.”




Kwa Upande wake Mgombea udiwani kata ya Hazina kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Lukanus Kayombo, ameahidi kuendeleza jitihada za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi mara atakapopewa ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo.


Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, Kayombo alisema uzoefu wake wa zaidi ya miongo mitatu akiwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kinyagwaroad, unampa ujasiri wa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Hazina kwa uadilifu na bidii.


Kazi yangu niliyoifanya nikiwa mwenyekiti mnaifahamu. Nimejenga ofisi ya serikali ya mtaa, nimewapatia wazee bima ya afya. Sasa mmeniongezea daraja, nawahakikishia hili daraja tutalifanya pamoja kwa vitendo,” alisema Kayombo.




Naye mgombea udiwani wa kata ya Zuzu, Jenesta Malingo, aliungana na wenzake kumuombea kura Kayombo akisisitiza umuhimu wa “mafiga matatu” yaani kura kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kura kwa mbunge Pascal Chinyele, na kura kwa diwani wa kata ya Hazina, Mhe. Kayombo.


Ikiwa mafiga yanahitajika matatu, basi figo la tatu ni baba yetu Kayombo. Tukimchagua, tutachapa kazi kweli kweli kwa maendeleo ya Hazina na Jiji la Dodoma, alisema Malingo.


Uzinduzi huo ulipambwa na shamrashamra za wananchi, huku washiriki wakiahidi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.







🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.


🚨Soma HABARI Zaidi katika BlogSpot yetu ya WASHINDI MEDIA.




Previous Post Next Post