KISHINDO CHA MARY CHATANDA MUSOMA MJINI, MKOANI MARA.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania UWT Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) Leo Tarehe 07 Septemba, 2025, apokelewa kwa Kishindo Musoma Mjini Mkoani Mara, tayari kwa kazi ya kufanya Kampeni ya kuwanadi Wagombea wa udiwani, Ubunge, pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Akizungumza na wanawake/wanachama wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini ambapo Jimbo la Musoma limemsimamisha Mwanamke katika nafasi ya Ubunge, Mgole Miraji Kigera, Huku Chatanda akiwataka Viongozi wa UWT Musoma Mjini kufanya Kampeni za Nyumba kwa nyumba, Mtaa kwa Mtaa, Kata kwa kata ili kuhakikisha Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wote wanaibuka na Ushindi wa Kishindo.






🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post