JANE CHITOJO AHAKIKISHA KUUNGA MKONO WENZAKE CCM DODOMA

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Septemba 5, 2025 – Katika uzinduzi wa kampeni za ubunge katika Kata ya Chang’ombe, wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao hawakupewa nafasi ya kupeperusha bendera, wameahidi kuunga mkono wenzao waliochaguliwa ili kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo katika jimbo la Dodoma Mjini.


Miongoni mwao ni Jane Chitojo, ambaye aliwahi kugombea kupitia viti maalum vya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoani Dodoma. 


Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Chitojo amesema kwamba licha ya jina lake kutajwa kwenye orodha ya wagombea, ni jukumu la kila mgombea kuunga mkono wenzao.


“Naweza kusema kwamba leo tumekuza kampeni katika jimbo la Dodoma Mjini, na tumeona wagombea wote waliopewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM wakiwa tayari kuinadi ilani ya chama. Hata sisi ambao hatukupata nafasi, jukumu letu ni kuwaunga mkono wenzetu kuhakikisha CCM inaendelea kubaki madarakani,” alisema Chitojo.



Chitojo aliongeza kwamba wagombea wote wanapaswa kushirikiana kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa Rais, wabunge, na madiwani. 


“Tunakwenda pamoja na Mh. Mbunge Paschal Chinyele, na tumekubaliana kuhakikisha Oktoba tutatoa tiki tatu kwa Mh. Rais, wabunge wetu, na madiwani,” alisema.


Akizungumzia kutajwa kwa majina yake kwenye orodha ya wagombea, Chitojo alisema, “Nilipoona jina langu halikuwepo, siku ile nilivunja makundi, lakini tayari nimejizatiti kwa kazi moja tu – kuhakikisha CCM inapata kura nyingi.”


Uzinduzi huo umeonesha mshikamano mkubwa miongoni mwa wagombea na wanachama wa CCM katika jimbo la Dodoma Mjini, ambapo wamesisitiza mshikamano wa kisiasa unaolenga kuimarisha nafasi ya chama katika uchaguzi wa Oktoba.







🚨Soma HABARI Zaidi katika BlogSpot yetu ya WASHINDI MEDIA.


🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post