WANAFUNZI WAPATIWA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU


Na Mwandishi Wetu, 
Dodoma.

Haki za binadamu  zinaendana na wajibu,

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uchunguzi Mkuu Bw. Fadhili Muganyizi wakati akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari  St Gabriel Tech walipotembelea Banda Tume ya Haki za Binadamu na    Utawala Bora katika Maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya  Nzuguni Jijini Dodoma.


Bw. Muganyizi amesema kuwa watoto wana haki ya kuishi, kusikilizwa, kutoa maoni, kupata taarifa na haki ya kupata elimu


"Haki zote ni muhimu kuzipata na THBUB  pia ina jukumu la kutoa elimu kwenu ili muweze kuzijua" amesema Bw. Muganyizi


Pia Bw. Muganyizi amewaeleza wanafunzi hao kuhusu wajibu wao wanapokuwa shuleni na katika Jamii kwani wao ni viongozi wa baadae.


"Pamoja na kuwa na haki ya kupata elimu, pia mna wajibu wa kusoma ili muweze kufaulu sambamba na kuheshimu jamii inayowazunguka ili kuwa viongozi bora wa  baadae" amesema Bw. Muganyizia 


Aidha, wanafunzi hao walielezwa pia majukumu ya THBUB ambapo pia walipata fursa ya kuuliza maswali kuhusu haki za binadamu  na utawala bora .


Kwa wapande wake Anthonia Vendeline Mwanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Shule hiyo  ameishukuru THBUB  kwa kuwapatia elimu hiyo  ambayo imewasaidia kutambua haki na wajibu wao sambamba na kuijua THBUB. 


"Tumefurahi, asanteni sana" amesema Anthonia


🚨Subscribe YOUTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post