Na Carlos Claudio, Dodoma.
Katika kuunga mkono juhudi za serikali kukuza sekta ya kilimo, Shirika la Bima la Taifa (NIC) linaendelea kutoa elimu na huduma za bima ya kilimo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane) yanayoendelea katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Mbeya, Lindi na Simiyu (Labora).
Kupitia ushirikiano wake na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), NIC imewezesha mafunzo kwa vijana 96 kutoka Mpango wa Building a Better Tomorrow (BBT).
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Banda la Mdhamini wa Maonesho – Coop Bank, Nzuguni Dodoma, yamelenga kuwajengea uwezo vijana katika elimu ya fedha, uwekezaji, bima za kilimo na maadili ya biashara.
NIC imeendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya sekta ya kilimo kwa kuhakikisha wakulima na wafugaji wanalindwa dhidi ya majanga kupitia bima ya kilimo, hivyo kuongeza tija na faida kwao.
Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la NIC lililopo kwenye Tenti ya Taasisi za Fedha (Agri-Financing Pavilion) ili kujifunza zaidi kuhusu faida za bima ya kilimo na jinsi inavyoweza kubadilisha maisha yao kupitia kilimo biashara.
🚨Subscribe YOUTUBE Channel yetu ya WASHINDIMEDIA