Na Jasmine Shamwepu, Dodoma.
TANZANIA imetajwa kuwa ni moja na nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, ambazo zimeathirika kwa sehemu kubwa na janga la Ukimwi ambapo hadi sasa inakadiliwa kuwa na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi milioni 1.7.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Samwel Sumba, amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye viwanja vya maonesho ya Wakulima Nanenane.
Aidha, Sumba amesema kuwa takribani asilimi 90 ya watu hao ambao ni zaidi ya milioni 1.5 wanapata huduma za matibabu ya kufubaza virusi vya ukimwi.
“Lakini sambamba na hayo lakini pia mafanikio mengi yamepatikana ikiwemo kuendelea kupungua kwa maambuzi ya virusi vya ukimwi kutoka zaidi ya watu 100,000 kwenye miaka ya 2000 hadi watu 60,000 kwa takwimu za mwaka 2023,"amesema
Pia, amesema kutokana na kuwapo kwa huduma za matibabu na mafunzo vifo viemendelea kupungua.
"Mtakumbuka miaka ya nyuma kabla ya kuanza kwa programu za matibabu na mafunzo ya kitaifa tulikua tunakadiliwa watu zaidi ya 100,000 walikuwa wanapoteza maisha kwa mwaka na kuugua lakini kutokana na uwepo wa huduma za matibabu na mafunzo vifo vimepungua hadi watu 25 kwa mwaka,"amesema
Vile vile, amesema Sambamba na hilo pia wamefanikiwa kupunguza maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto kwa kiasi kikubwa.
Amesema kabla ya kuanza kwa programu za kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto maambukizi yalikuwa takribani zaidi ya asilimia 42.
"Lakini yameshuka mpaka asilimi 7.6 kwa mwaka 2024 hii inamaana gani ni kuwa kila akimama 100 wanaoishi na virusi vya ukimwi kabla ya huduma za kuzuia maambuzi ya mama kwenda kwa mtoto watoto 42 walikuwa wanapata maambukizi lakini hivi sasa ni watoto saba tuu,"amesema
Kadhalika, amesema wamefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa hali ya unyanyapaa ambayo ndiyo kikwazo kikubwa katika upatikanaji wa huduma.
"Kulikuwa na programu mbalimbali za elimu kwa jamii serikali ikishirikina na wadau mbalimbali wa maendeleo na kwa takwimu za mwaka 2023 unyanyapaa ulikuwa unakadiliwa kufikia takribani asilimia 28 lakini hadi takwimu za 2024 ulikuwa kwenye asilimia tano,"amesema
Mbali na hilo amesema wanaipongeza serikali kwa kuendelae kuboresha huduma za Ukimwi, hususani huduma za kinga, matibabu na matunzo.
Hata hivyo amesema kwa mwaka wa fedha ujao serikali imetenga takribani bilioni 277 fedha ndani kwa ajili ya kuwekeza kwenye mfuko wa udhamini wa ukimwi hali itakayo saidia kupunguza utegemezi wa ufadhili kutoka nje kwa ajili ya huduma za Ukimwi.
"Tunatoa rai kwa wanachi kuwa janga la Ukimwi bado lipo huduma zipo watu wapime na wale watakao gundulika waanze kutumia dawa na wanaotumia dawa wawe wafuasi wazuri wa huduma hizo za matibabu,"amesema
🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA