Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam.
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetaja mafanikio yake katika miaka saba ya uwepo, ukiwemo ulipaji wa jumla ya shilingi trilioni 11.96 kwa wanachama 348,909.
Meneja wa Mafao wa PSSSF, Ramadhani Mkenyenge, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao ni wanachama wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania MISA TAN, kutoka maeneo mbalimbali nchini waliokutana Jijini Dar es salaam.
Akasema mfuko huo ulianzishwa Agosti 1, 2018 ukiwa na wanachama 862,986 na hadi Juni 30, 2025 una jumla ya wanachama hai 807,010.
Aidha akasema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, PSSSF inalenga kukusanya wastani wa shilingi bilioni 168.25 kwa mwezi, sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 43 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa Meneja huyo wa Mafao wa PSSSF huduma nyingi sasa zinapatikana kidijitali ili kuwaondolea wanachama usumbufu wa foleni na kusafiri hadi ofisini.
Naye Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema mashirikiano kati ya PSSSF na wanahabari yataendelea kuimarishwa ili kuhabarisha umma kuhusu huduma za hifadhi ya jamii.
🚨Subscribe YOUTUBE Channel Yetu Ya WASHINDI MEDIA.