GST yaonesha fursa za uwekezaji kwenye madini ya kutengeneza mbolea nchini

 


Yasisitiza taarifa zitokanazo na tafiti zake zina manufaa katika sekta nyingi.

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeeleza wadau kupitia maonesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma kuwa Tanzania ina utajiri madini kilimo yanayotumika kutengenezea mbolea


Hayo yamebainishwa leo tarehe 03/08/2025 leo na Mjiolojia Mwandamizi kutoka GST ndugu Hamis Ramadhani. Bw. Hamisi alielezea ramani ya Tanzania  inayoonesha uwepo wa madini ya kutengeneza mbolea yanayopatikana katika maeneo mbalimbali nchini. 


 Bw. Hamisi alieleza baadhi ya madini kilimo yanayopatikana nchini Tanzania ni pamoja na Bentonite, Diatomite, Dolomite, Gypsum, Limestone, Kaolin na Phosphate.


Bw. Hamisi alieleza kuwa madini hayo sio tu yanatumika kutengeneza mbolea lakini yapo ambayo yanasaidia kupunguza au kurekebisha kiwango cha tindikali katika udongo na hivyo kuboresha afya ya udongo kwa uzalishaji wenye tija wa mazao. 


 Bw. Hamisi alifafanua kuwa tafiti za madini zinazofanywa na GST hazilengi  kuchochea uwekezaji kwenye Sekta ya Madini tu bali hata sekta nyinginezo kama Kilimo, Maji, Nishati na Ujenzi. 


Bw. Hamisi alitoa wito kwa wadua wote kutumia taarifa zinazotokana na tafiti za madini zinazofanywa na GST ili kuongeza tija katika shughuli za kilimo, utafutaji na uchimbaji maji, shughuli za ujenzi na shughuli za utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji madini.





🚨Subscribe YOUTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA

Previous Post Next Post