Na. Wellu Mtaki, Dodoma.
Afisa Michezo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Evance Sangawe, amesema kuwa mkoa wa Dodoma unajipanga vyema kushiriki mashindano ya UMISSETA kitaifa ambapo mashindano Hayo yanatalajia kufanya kuanzia Tarehe 20 Hadi 30 juni Mkoani Iringa huku timu ya wachezaji 120 walioteuliwa baada ya mchujo wa kina kutoka kwa washiriki wa mashindano ya ngazi ya mkoa itaingia kambini kwa siku saba kabla ya kuelekea Iringa.
Hayo ameyasema wakati wa hafla ya kufunga mashindano iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Dodoma ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa elimu kutoka ngazi ya wilaya na mkoa.
Aidha amesema kiwa uteuzi wa walimu watakao fundisha kambini umezingatia utendaji kazi wao kwenye mashindano ya mkoa na uzoefu katika mashindano ya kitaifa.
" Mkoa tumejipanga kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana. Walimu walioteuliwa wana uzoefu wa kitaifa na tumeandaa programu maalum ya mazoezi na maandalizi ya kisaikolojia kwa vijana wetu,” amesema hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa timu hiyo ya mkoa" amesema Sangawe
Naye Mchumi wa Mkoa wa Dodoma Charles Mduma aliyemwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo Kaspar Mmuya amewasihi wawakilishi wa mkoa huo kutobweteka bali kujiandaa kikamilifu kwa mashindano ya kitaifa huku akiwataka wandindani wa Wilaya hiyo waliokosa nafasi ya kushiriki mashindano ya kitaifa wasikate tamaa bali wajitathimini na wajipange upya kwa mashindano yajayo
" Nawasihi mujipange vinzuri Ili mashindano ya kitaifa miludi na ushindi ni jambo la kujivunia kupata washiriki ambao watakwenda kuwakilisha mkoa na wale waliokosa nafasi awamu hii tumieni Muda vinzuri Katika kujipanga awamu zijazo ila msijisikie vibaya kwa kikao awamu hii " amesema Muda.
Nao baadhi ya wanafunzi walioteuliwa kuiwakilisha Dodoma ambao ni Iddi Yusuphu na Ester Robert wameeleza furaha yao na kuahidi kufanya vinzuri kuhakikisha mkoa wao unapata ushindi .
"Tunaamini tutafanya vizuri. Tumejifunza mengi kutoka kwa walimu wetu na na tunaendelea kujifunza Katika siku hizo za mafunzo tutakazokuwepo pia mashindano ya mkoa yamekuwa chachu ya mafanikio yetu naamini bendela tutaipeperusha kwa kishindo huko Iringa" esema mmoja wa wanafunzi hao.
Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya mashindano Hayo ni "Uongozi Bora ni Msingi wa maendeleo ya taaluma,Sanaa na Michezo,Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025 Kwa Amani na Utulivu.
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.