TIRA YAZINDUA KAMPENI YA NIC KITAA ZANZIBAR KUIHAMASISHA JAMII KUHUSU BIMA



Zanzibar.


Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Bi. Khadija Said amezindua rasmi kampeni ya NIC Kitaa Zanzibar yenye lengo la kuongeza uelewa wa bima kwa wananchi.


Bi. Khadija amesema "utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka 10 wa sekta ya Fedha, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ina majukumu mbalimbali iliojipangia ikiwemo jukumu la kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 uelewa wa bima uwe umeongezeka anagalu asilimia 30"


Kwa upande wa NIC Meneja wa Zanziba Bw. Hamis Msami akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Kaimu Abdi Mkeyenge amesema "NIC imekuwa wajibu wa kuhakikisha elimu na huduma za bima zinawafikia wanachi wote kupitia program mbalimbali ikiwemo vyombo mbalimbali vya habari kama vile CLOUDS TV/Radio na TVE/ E-fm ambavyo tunashirikiana kuandaa vipindi mbalimbali vya kuelimisha jamii"


Pia Bi. Khadija amesema jukumu lingine la Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kuwa ifikapo mwaka 2030 tuhakikishe kwamba asilimia 50 ya wananchi wanatumia huduma za bima."


Kampeni ya NIC Kitaa Zanziabar imeanza tarehe 23/06/2025 na itapita kwenye maeneo mbalimbali (Unguja na Pemba) na kuhitimishwa tarehe 06/07/2025




🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post