SERIKALI YAANZA MAANDALIZI YA UJENZI WA BARABARA YA MCHEPUO MLIMA NYOKA.



Na Saida Issa,Dodoma.


Serikali imethibitisha kuwa imeanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Mlima Nyoka kutoka Uyole hadi Songwe yenye urefu wa kilometa 48.9 kwa kiwango cha lami, ili kupunguza msongamano na kuboresha usafiri wa barabara katika maeneo hayo.


Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi David Kihenze alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini, Mheshimiwa Oran Manase Njeza,alipouliza Je, lini Serikali itajenga Barabara ya mchepuo ya Mlima Nyoka kutoka Uyole hadi Songwe


Amesema kuwa tayari kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa mradi huo imekamilika, hatua inayotoa msingi thabiti kwa kuanza kwa ujenzi wenyewe.


Kwa sasa, Serikali inaendelea na mchakato wa kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo muhimu, ambapo njia mbalimbali za upatikanaji wa rasilimali zinazingatiwa, ikiwemo kushirikiana na Sekta Binafsi kupitia mfumo wa Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP).


Barabara hiyo ya mchepuo inatarajiwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Uyole, Songwe na maeneo jirani, kwa kuwa itaondoa kero ya foleni na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa bidhaa na watu.




🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post