SACP KATABAZI APEWA TUZO YA HESHIMA NA MAAFISA USAFIRISHAJI

 


Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi amekabidhiwa tuzo ya heshima na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Waziri wa Madini Mh. Antony Mavunde kwa kutambua mchango wake Katika Jamii.


Hafla ya kukabidhiwa Tuzo hiyo imefanyika katika uzinduzi wa ofisi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) ya umoja huo Juni 10, 2025.


Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Umoja wa Madereva Pikipiki (bodaboda) na Bajaji Mkoa wa Dodoma (UMAPIDO) Mbunge huyo amesema Tuzo hiyo ni maalumu kutokana na juhudi kubwa anazozifanya Kamanda Katabazi za kupambana na wahalifu.


Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo SACP Katabazi Amewataka wananchi  kuendelea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kukomesha uhalifu unaorudisha nyuma maendeleo katika Jiji la Dodoma.








🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post