RAIS SAMIA KUFUNGUA KIWANDA CHA MBOLEA CHA DOLA MILIONI180 DODOMA.


Na Carlos Claudio Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea cha Itracom Fertilizers Limited itakayofanyika Juni 28, 2025, jijini Dodoma.


Kiwanda hicho kina thamani ya uwekezaji wa dola milioni 180 na kinatarajiwa kuongeza tija katika sekta ya kilimo nchini.


Akizungumza leo Juni 11, 2025 Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, amesema kiwanda hicho tayari kimezalisha ajira 1,805 kwa Watanzania.


Aidha, ameeleza kuwa wafugaji wa ng’ombe wameanza kunufaika kwa kuuza samadi, ambapo tani 11,000 tayari zimenunuliwa na kiwanda hicho kwa ajili ya uzalishaji wa mbolea.


“Wafugaji wa ng’ombe wamepata soko la uhakika la kuuza samadina mpaka sasa tani 11,000 ya samadi imeshanunuliwa” amesema Waziri Bashe.


Hii ni hatua kubwa katika kuinua uchumi wa kilimo na mifugo, huku ikisaidia kuongeza kipato cha wananchi na kupunguza gharama ya pembejeo nchini.






🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post