JE, KUNA MKAKATI GANI WA KUONGEZA UZALISHAJI NA UPATIKANAJI WA SOKO LA ZAO LA PARETO.

 


Na Saida Issa, Dodoma.


NAIBU Waziri wa  Kilimo David Silinde amesema kuwa Serikali katika mwaka 2024/2025 imetekeleza mikakati mbalimbali ili kuongeza uzalishaji wa zao la pareto nchini ikiwemo kusambaza mbegu bora kilo 890 za pareto kwa wakulima 3,500 katika maeneo ya uzalishaji na kuboresha mifumo ya upatikanaji wa soko kwa kusajili Kampuni 11 za kununua na kuchakata pareto.


Naibu huyo ameeleza hayo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza Je, kuna mkakati gani wa kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa Soko la Zao la Pareto.


Serikali katika mwaka 2025/2026 imepanga kuongeza uzalishaji wa pareto kufikia tani 5,000.


"Lengo hilo litafikiwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo kusambaza mbegu bora za pareto kilo 5,300 kwa wakulima, kutoa mafunzo kuhusu kanuni za kilimo bora cha zao la pareto kwa wakulima viongozi 19,000 na wakaguzi wa pareto 50 na kuratibu ujenzi wa makaushio 150 ya pareto katika Halmashauri za Makete, Ileje, Mbeya, Ludewa, Mbulu na Arusha,"amesema.





🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post