Na Carlos Claudio, Dodoma.
Sakata la mchezo nambari 184 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba ulioahirishwa Tangu Machi 08 mwaka huu limeuteka mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambapo wabunge wametaka Mamlaka zinazohusika na usimamizi wa mpira wa miguu nchini kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu.
Baaada ya hotuba za uwasilishaji wa bajeti ya Wizara hiyo pamoja na Taarifa ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo wabunge walipata wasaa wa kuchangia ambapo kila aliyesimama hakuacha kuugusia mchezo huo
Wameenda mbali zaidi wakimtaka waziri kutoa taarifa za kikao chake na viongozi wa vilabu hivyo pamoja na mamlaka za soka kilichofanyika Dar es salaam siku chache baada ya mchezo huo kuahirishwa.
Itakumbukwa hivi karibuni bodi ya Ligi kuu TPLB imetoa marekebisho ya ratiba ya michezo ya ligi kuu ikiupangia mchezo huo kupigwa Juni 15 mwaka huu.
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.