Na : Stella Ngenje-Songea.
Wananchi Wilayani Rufiji Mkoani Pwani wametakiwa Kujitokeza kwenye Vituo vya Kupigia Kura ili kujiandikisha nakuboresha Taarifa zao kwenye Daftari lakudumu la Mpigakura litakapowafikia kwa awamu ya pili,akiwasihi pia kujitokeza kupigakura Baadae Mwaka huu.
Ameyasema hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania UWT Ndg.Mary Chatanda (MCC) akiwa Ziarani Mkoani Pwani ,ametumia nafasi hiyo kuhamasisha Wanawake Kujiandikisha, "Hamasisheni Wanaume wajiandikishe, na Vijana Wajiandikishe ili ikifika siku yakupigakura Octoba wampigie Dkt. Samia, Wanaosema Uchaguzi Hautakuwepo wanapoteza muda tunawaomba Wala wasijisumbue Dkt.Samia Mitano Tena".
Akiwa Rufiji Chatanda ameeleza Mafanikio Makubwa yaliyoletwa na Serikali ya awamu ya Sita ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ameimarisha Sekta Mbalimbali ili kuondosha adha kwa Wananchi wa Rufiji, Mathalani Kwenye Sekta ya Elimu,Afya,Maji Miundombinu ya Barabara Sambamba na uwezeshaji Wananchi kiuchumi.
Ziara hii Mkoani Pwani pamoja na Mambo Mengine, Chatanda amesema inalenga Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM, akimtaja Dkt. Samia Kuwa ni "Mwanamke na Nusu" na kwamba anastahili Pongezi kwa Maendeleo Makubwa aliyoyaleta kwa Mikoa Mbalimbali hapa Nchini, Ikiwemo na Mkoa wa Pwani.
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.