RAIS SAMIA ATANGAZA KIFO CHA MEE CLEOPA MSUYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais a Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Cleopa David Msuya.


Rais Dkt. Samia amesema kuwa kifo hicho kimetokea leo, Jumatano Mei 07.2025 saa 3 asubuhi katika Hospitali ya Mzena, jujini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.


"Hayati Cleopa David Msuya ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu ndani na nje ya nchi ikiwemo katika Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Hispitali ya Mzena na kule jijini London" -Rais Dkt. Samia.


Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu zake za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo na kutangaza siku saba za Maombolezo kitaifa.


🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post