TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA NISHATI NA NCHI ZA NORDIKI — MHE. MRAMBA

 


Na Wellu Mtaki, Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi za Nordiki ambazo ni Denmark, Finland, Norway na Sweden katika kuangalia fursa zilizopo katika uzalishaji wa nishati .


Mhe. Mramba ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Nordiki 2025 inayofanyika kuanzia Mei 26 hadi 29, 2025 ambapo maadhimisho Hayo  yanaadhimishwa  Mkoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro.


Aidha, amesema eneo lingine ni uwekezaji katika miradi ya uunganishaji wa umeme katika nchi moja kwenda nchi nyingine ambapo kwasasa Tanzania inataka kuunganisha na nchi jirani.


Amesema tangu uhuru mataifa hayo yamekuwa yakishirikiana na Tanzania kwenye eneo la nishati pamoja na kutoa mikopo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kusambaza umeme nchini.


🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post