JKT YATOA WITO KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA 2025 KUJITOKEZA KWENYE MAFUNZO YA KIJESHI

 


Na. Wellu Mtaki, Dodoma.


Mkuu wa jeshi la kujenga Taifa Meja Jenerali Nduku Mabele ametoka wito kwa vijana waliohitimu Elimu ya  kidato Cha sita kwa Mwaka 2025 kutoka shule zote za Tanzania bara kuhudhuria mafunzo ya JkT kwa mujibu wa Sheria kwa Mwaka huu.


Hayo ameyasema Kanali Juma Mlai Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu wito wa  kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria Mwaka 2025.


Amesema jeshi la kujenga Taifa limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia Mei28, 2025 hadi Mei 8,2025.


Aidha amesema kuwa orodha ya  majina, makambi waliyopangiwa na vifaa vinavyotakiwa vinapatikana Katika tovuti ya JKT ila wahitimu wenye ulemavu  waripoti Katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani .


🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post