Na Carlos Claudio, Dodoma.
Madereva wa serikali wametakiwa kuzingatia sheria za barabarani pindi wanapotumia vyombo vya moto ili kuepusha ajali zitokanazo na uzembe wa kuto tii sheria.
Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Jesho la Polisi Mkoa wa Dodoma ikiingozwa na kamanda wa polisi mkoa huo SACP George Katabazi wakati wa kikao na madereva wa serikali kilicholenga kujenga uhusiano wa karibu kati ya jeshi la polisi na madereva wa taasisi mbalimbali.
Kamanda Katabazi amesema jeshi la polisi halitosita kuwachukulia hatua sitahiki madereva wote watakao kiuka sheria za barabarani huku akiwahimiza kuwa,kuwa derava wa serikali haimanishi kuvunja sheria za barabarani.
"Nawakemea wale ambao kwa makusudi wanavunja sheria za barabarani kisa ni dereva wa serikali ni watake kila mmoja azingatie sheria,kanuni na taratibu za barabarani.
"Kikao hiki kitadumisha uhusiano baina ya jeshi la polisi Dodoma na madereva wa serikali kwani wote ni watumishi wa serikali lazima tushirikiane kuthibiti uhalifu barabarani na kuzuia ajali za barabarani,"amesema.
Aidha Kamanda Katabazi ametumia kikao hicho kuwakumbusha waendeshaji wote wa vyombo vya moto kuwa hakuna aliyeko juu ya sheria hivyo basi sheria haitobagua atakaye sanabisha ajali barabarani kulingana na wadhifa wake katika jamii.
Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma ( SACP) George Katabazi na makundi mbalimbali katika mkoa huo vyote vikilenga kuleta ushirikiano wa jeshi la polisi na makundi mbalimbali kwaajili ya kuweza kuzuia uhalifu katika mkoa huo.
Nae mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dodoma Yusuphu Kamota amesema wanafanya ukaguzi (oparesheni) mara kwa mara ya ukamataji wa makosa hatarishi pamoja na kutoa elimu ili kuhakikisha hali ulya usalama ndani ya mkoa wa Dodoma inakuwa shuari
Amesema jeshi la polisi limekuwa likifanya oparesheni ya kuondosha namba za magari ambazo siyo rasmi iliwemo chases namba pia ikizingatia l kifungu cha usalama barabarani namba 54 kinachoeleza aina ya magari yanayotakiwa kufungiwa vimulimuli pamoja na vin’gola.
“Tumewakamata madereva zaidi ya 30 wengine ni madereva wa serikali, idara zengine pamoja na watu binafsi wakiweka hivi vimulimuli na vin’gola pamoja na namba zisizokuwa rasmi, katika hao tuliowakamata wapo tuliowapeleka mahakamani na kesi zao zinaendelea,” amesema Kamota.
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.