Na Carlos Claudio, Dodoma.
Katika kuelekea kilele cha Siku ya Kantate inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Mei, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Dodoma, Jimbo la Makao Makuu, limeadhimisha tukio hilo kupitia utumbuizaji wa kwaya mbalimbali.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Ushirika wa Arusha Road, yakihusisha kwaya 19 kutoka Jimbo la Makao Makuu, ikiwemo kwaya ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kwaya kutoka Ilula, Iringa, ambazo zote zilitoa burudani ya kipekee kwa miondoko ya Kantate Domino
Akizungumza katika maadhimisho hayo Askofu wa Dayosisi ya Dodoma Mhe. Askofu Dkt. Christian Ndossa, amesema kuwa muziki wa kantate ni sehemu muhimu ya ibada na maisha ya kiroho ya Wakristo huku akinukuu maandiko kutoka kitabu cha Zaburi 150:6
Kantate Domino ni aina ya muziki wa kwaya unaotumika kuabudu na kumtukuza Mungu kwa utaratibu wa kipekee na wenye mizani ya kiroho ya juu.
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.