KIJIJI CHA NYUKI CHABUNI MIZINGA YA KISASA YENYE MAJI, YALETA MAPINDUZI KATIKA UFUGAJI WA NYUKI


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Kampuni ya kijiji cha nyuki kupitia tafiti imebuni na kutengeneza mizinga ya nyuki ya kibiashara yenye maji pembezoni ili kukata safari zinazotumiwa na nyuki hao katika kuchota maji na kuongeza nguvu katika malisho ya nyuki yanayopelekea ongezeko la uvunaji kwa mfugaji.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji cha Nyuki Philemon Kiemi katika Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani, ambayo kitaifa yamefanyika katika Kiwanja cha Chinangali jijini Dodoma  huku akifafanua mazao mbalimbali yanayovunwa kupitia nyuki ikiwemo sumu, gundi , maziwa na mengineyo.


Sambamba na hayo Kiemi amesema kampuni ya kijiji ipo teyari kuwekeza katika sekta ya utalii kanda ya kati huku akitoa ushauri kwa serikali kubadilisha miundombinu ili kampuni hiyo iweze kutangaza utamaduni pamoja na kuuza utamaduni wa mtu wa kanda ya kati kwa manufaaa ya taifa.


Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani kwa mwaka huu inasema ‘Nyuki kwa Uhai na Uchumi Imara, Tuwahifadhi’







🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post