MAADHIMISHO SIKU YA ZIMAMOTO YAPAMBA MOTO MKOANI DODOMA



Dodoma.


Kuelekea kilele cha wiki la zimamoto, Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji Dodoma wamerudisha fadhila zao katika jamii kwa kuonesha matendo ya huruma katika kituo cha afya cha Makole ambapo wamefanya usafi na kuchangia damu katika kituo hicho lengo ikiwa kujali na kuokoa maisha ya mtanzania kama ilivyo dhamira ya jeshi hilo katika kuokoa mali na maisha ya mwananchi.


Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma wamefanya usafi pamoja na kuchangia damu kwenye Kituo cha Afya Makole kilichopo Jijini Dodoma leo Mei 3, 2025


Zoezi hilo la usafi na uchangiaji damu limeongozwa na Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Dodoma Mrakibu (SF) Rehema Menda ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya Siku ya Zimamoto Duniani Mei 4, 2025.


Naye Afisa Muuguzi Msaidizi Fransisca Mrosso kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya amelishukuru sana Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa huduma waliyoitoa katika Kituo hicho






















Dunia itaadhimisha Siku ya Zimamoto Mei 4, 2025 kwa lengo la kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha wakati wakipambana na Moto wa nyika Nchini Australia mwaka 1999.


🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.


Previous Post Next Post