JULIUS MWITA AWASILISHA UTETEZI WAKE CHADEMA

 


Aliyekuwa mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Musoma Mjini mwaka 2020, Julius Gabriel Mwita, ameibuka na majibu mazito dhidi ya barua ya Katibu wa CHADEMA Tawi la Nyabisare iliyomtaka kujieleza kwa nini anadaiwa kwenda kinyume cha misimamo ya chama, ikiwemo ajenda ya No Reforms No Election.


Katika barua ya tarehe 01 Mei 2025, Katibu wa Tawi la Nyabisare kata ya Bweri, jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara, alimwandikia Mwita akimtaka kuandika maelezo ya kujieleza na pia kufika mbele ya Kamati ya Utendaji ya Tawi hilo tarehe 14 Mei 2025. Barua hiyo ilimlaumu Mwita kwa "kupotosha misimamo ya chama" kupitia mitandao ya kijamii na "kukiuka maadili ya viongozi" kwa mujibu wa Kanuni za CHADEMA.


Barua hiyo ya CHADEMA ilidai kuwa taarifa mbalimbali kutoka maeneo tofauti zilibainisha kuwa Mwita alikwenda kinyume cha misimamo ya chama kwa kuchapisha na kusambaza maoni yake binafsi yasiyolingana na msimamo rasmi wa CHADEMA kuhusu uchaguzi, bila ridhaa ya vikao halali vya chama.


Hata hivyo, katika barua yake ya majibu ya Mei 6, 2025 ambayo Jambo TV tumepata kuiona, Mwita ameeleza kuwa hakuwahi kuwa kiongozi wa chama kwa ngazi yoyote kwa sasa, hivyo kutumia kanuni zinazohusu "maadili ya viongozi" ni kumkosea haki

waziwazi.


Mwita amelalamikia pia utaratibu wa kupelekewa barua kwa njia ya WhatsApp, akisema si rasmi kikatiba, na kudai kuwa barua hiyo ilisambazwa katika makundi ya mitandao ya kijamii kwa malengo ambayo ameeleza kutoyafahamu.


🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post