Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania UWT *Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC)* amehitimisha ziara yake Wilayani Rufiji kwa Kufanya Mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Ujamaa amewasihi Wananchi wa Rufiji kutowaozesha watoto wakike mapema badala yake wajikite katika kuwahimiza kuzingatia masomo yao ili waje kutimiza ndoto zao za kielimu.
Chatanda aliyeambatana na Makamu Mwenyekiti wa UWT *Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC)* Wajumbe wa NEC, na Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT, amesema Serikali kupitia Mbunge wa Rufiji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa imefanya mambo mengi ya kimaendeleo katika Sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu pamoja na Uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa kuwapatia mikopo yenye Riba nafuu ili kuwainua kiuchumi.
Pamoja na mambo mengine Chatanda, akawakumbusha wananchi wa Rufiji kujitokeza kwenye uboreshaji wa taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea sasa kwa awamu ya pili ili wawe na sifa ya kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwezi Oktoba, 2025.
#UWTImara
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#UWTZiaraPwani
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.