BASHE: WAUZA MBEGU FEKI NI WAUWAJI – SHERIA KUBWA YAJA

 


Na Carlos Claudio, Dodoma.


Waziri wa kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema wizara itabadilisha sheria ya TARI, TOAST, TPHPA na TFRA kwa yeyote anayekamatwa anauza mbegu, kiwatilifu au mbolea feki atawekwa katika kundi la wahujumu uchumi.


Waziri Bashe Ameyasema hayo leo jijini Dodoma katika mkutano wa Taifa wa wadau wa Tasnia ya Mbegu huku akiwafananisha wauza mbegu feki kama wauwaji.


Aidha Waziri Bashe amewataka wasambazaji wa mbegu nchini kuhakikisha kuna upatikanaji wa mbegu ambazo ni nafuu kwa mnunuzi kisha ndipo wazungumzie suala la Shikizo la kemikali juu ya mbegu yaani (adoption) of seeds kwakuwa suala hilo la adoption linahitaji mafunzo.


Hizi ni taasisi muhimu katika sekta ya kilimo nchini Tanzania. Hapa chini ni majina yao kamili:

  1. TARI – Tanzania Agricultural Research Institute (Taasis ya Utafiti wa Kilimo Tanzania)
  2. TOAST – Tanzania Official Seed Certification Institute (Taasis ya Uthibitishaji wa Mbegu Tanzania)
  3. TPHPA – Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania)
  4. TFRA – Tanzania Fertilizer Regulatory Authority (Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania)

Zote zina jukumu muhimu katika kuhakikisha ubora na usalama wa pembejeo za kilimo kama mbegu, viuatilifu, na mbolea.





🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post