Na. Hellen M. Minja,DODOMA RS.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amekutana na viongozi wa makundi mbalimbali yanayopatikana katika Mkoa huu leo Mei 15, 2025 katika ukumbi wa ofisi yake iliyopo jengo la Mkapa Jijini Dodoma.
Lengo la makutano hayo ni kuzungumzia mambo tofauti tofauti yanayohusiana na Mkoa ikiwa ni pamoja na kuwasisitiza kuhakiki na kuhuisha majina yao kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga kura zoezi lililokwisha anza ili wawe na sifa za kushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka huu 2025.
Aidha, Mhe. Senyamule alizungumzia vipaumbele vya Mkoa ambavyo ni kilimo cha matunda hasa ‘Apples’, Utalii, Madini, Mji wa kilojistiki, Viwanda na Biashara pamoja na kujiandaa na maandalizi ya ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopewa jina la ‘Samia Day’ anayotarajia kuifanya Mkoani hapa Mwezi Juni, 2025.
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.