CHANZO CHA PICHA,REUTERS.
Umma waruhusiwa kuingia Basilica ya St Peter kumuona Papa.
Waombolezaji wameanza kuwasili katika Kanisa kuu la St Peter's Basilica kutoa heshima zao za mwisho kwa Papa Francis.
Kanisa hilo litasalia wazi hadi 24:00 saa za eneo (23:00 BST) leo.
Jeneza la Papa limewekwa mbele ya Madhabahu ya Kipapa
Hapa kuna picha ya jeneza la Papa, lililo ndani ya Basilica kuu ya St Peter, mbele ya Madhabahu ya Kipapa - ambayo imejengwa juu ya kaburi la mtakatifu.
Itabaki hapo hadi mazishi siku ya Jumamosi.
Watu wanaendelea kumuomboleza Papa Francis kote duniani.
Watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanaendelea kumuomboleza Papa Francis.
Katika picha zifuatazo, tunaweza kuona hisia zikiongezeka katika kwenye uwanja wa St Peter's Square walipokutana asubuhi ya leo, pamoja na watu wakitoa heshima zao kwa marehemu papa huko Jerusalem na Jakarta.
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.