CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES.
Marcus Rashford anahisi kwamba kuna uwezekano mdogo wa kuichezea Manchester United tena chini ya Ruben Amorim, lakini hataharakishwa kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake.
Rashford alifunga bao lake la nne tangu ajiunge na Aston Villa kwa mkopo mnamo Februari katika mechi waliopoteza 2-1 dhidi ya Manchester City Jumanne.
Mkataba wa mkopo wa mshambuliaji huyo huko Villa Park unamalizika mwishoni mwa msimu.
Lakini wakati mkataba wake United unatarajiwa kumalizika 2028, na sio kwamba hakuna uwezekano wa Rashford kurejea, vyanzo vya karibu na mchezaji huyo hawaoni haja ya kurejea Old Trafford.
Rashford alitolewa na Amorim kutoka kikosi cha kwanza tangu mwezi Desemba, kisha, kando na kushindwa nyumbani huko Newcastle mnamo 30 Desemba alipokuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika, hakumchagua tena katika kikosi chake.
Kufuatia kuhama kwa Villa, Amorim alisema: "Sikuweza kumfanya Marcus aone jinsi anavyotakiwa kucheza soka na kumfunza jinsi ninavyoiona."
Inamaanisha kuwa United italazimika kuamua ama kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 au kumwacha aondoke kwenye klabu hiyo kwa mkataba mwingine wa mkopo msimu huu.
Huku United - na Amorim - wakijaribu kubana na kubambanya masuala ya fedha ili kuunda upya kikosi ili iendane na mtindo wa uchezaji wa bosi huyo wa zamani wa Sporting, kuwa wazi juu ya mchezaji huyo ambaye ni kati ya wanaolipwa pesa nyingi litakuwa jambo lenye tija.
Hata hivyo, uwezekano ni mdogo.
Rashford ameondoa uwezekano wa kuhamia London, ambapo angejiunga na klabu ambayo imefuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
Vyanzo vya karibu na mchezaji huyo vinasisitiza kuwa Rashford bado hajazungumza kuhusu mustakabali wake na hana mpango wa kufanya hivyo hadi katikati ya Juni.
Hata hivyo, inafahamika kuwa hana nia ya kuwa sehemu ya mpango wa kubadilishana wachezaji - baada ya uvumi wa hivi majuzi kuhusu nia ya United kumnunua mshambuliaji wa Crystal Palace Eberechi Eze.
Rashford sasa hivi anavutia wengi zaidi kuliko alivyokuwa alipojiunga na Villa tarehe 2 Februari.
Ingawa mabao manne katika mechi 17 hayawezi kuchukuliwa kuwa mengi, mchango wake kwa ujumla - ikiwa ni pamoja na pasi za mabao sita - kwa Villa yamekuwa na mchango mkubwa.
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.