CHANZO CHA PICHA, GALLO IMAGES.
Mchezaji wa Durban City, Sinamandla Zondi
Mchezaji kandanda wa Afrika Kusini, Sinamandla Zondi amefariki Jumanne baada ya kuzirai wakati akiwa uwanjani akijiandaa na timu yake kucheza mechi ya daraja la pili, imesema klabu yake ya Durban City.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alipelekwa hospitalini kabla ya mchezo wa Durban dhidi ya Milford FC na mechi ilisitishwa wakati wa mapumziko baada ya maafisa kuambiwa Zondi amefariki.
"Kwa huzuni kubwa tunathibitisha kifo cha Sinamandla Zondi, almaarufu Sgora, mchezaji pendwa wa Durban City," klabu hiyo imeema katika taarifa.
Beki huyo alicheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa Septemba 2021 na amecheza mara kwa mara katika klabu yake msimu huu, wakiwa kileleni mwa msimamo na wako mbioni kupandishwa kwenye ligi kuu ya soka ya Afrika Kusini.
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.