VANCE ASEMA MAREKANI `ITAJIONDOA’ LABDA UKRAINE NA URUSI ZIFIKIE MAKUBALIANO.

 


CHANZO CHA PICHA,REUTERS.


Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amesema nchi yake "itajiondoa" isipokuwa Ukraine na Urusi zifikie makubaliano akirejelea maoni ya hivi karibuni kutoka kwa maafisa wa Marekani.


Vance ametolewa onyo hilo baada ya mazungumzo ya London kati ya maafisa kutoka Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ukraine na Marekani yaliyolenga kufikia usitishaji mapigano, kupungua makali baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio na mjumbe maalum Steve Witkoff kujiondoa.


Marekani inaangazia mazungumzo ya wiki hii mjini Moscow, ambapo Witkoff atakutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa mara ya nne, huku kasi ya diplomasia ya kumaliza vita ikiongezeka.


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, wakati huo huo, alisema anasisitiza "kusitishwa kwa mapigano mara moja, kabisa na bila masharti".


"Kukomesha mauaji ni kipaumbele cha kwanza," Zelensky alisema kwenye mtandao wa kijamii Jumatano.


Matamshi yake yanawadia huku Vance akiwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini India kwamba Marekani imetoa "pendekezo la wazi" kwa Warusi na Waukreni.


"Ni wakati wa wao kusema ndiyo au Marekani ijiondoe katika mchakato huu," aliongeza. "Tumejishughulisha na diplomasia ya kipekee kama msingi."


Mjumbe wa Trump wa Ukraine, Jenerali Keith Kellogg, anahudhuria mazungumzo hayo mjini London badala ya Witkoff na Rubio, ambao walitaja mazungumzo ya Jumatano kama "mikutano isiyo rahisi".


🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.

Previous Post Next Post