CHANZO CHA PICHA, REUTERS.
Mahmoud Abbas amewaita Hamas "watoto wa mbwa" katika hotuba iliyojaa maneno kali ambapo alilitaka kundi hilo kuwaachilia mateka ambao bado inawashikilia, kuachana na silaha na kukabidhi udhibiti wa Gaza ili kumaliza vita na Israel.
Rais wa Mamlaka ya Palestina aliuambia mkutano katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu kwamba Hamas imeipa Israel "visingizio" vya kuendeleza mashambulizi yake dhidi ya Gaza, na kuliambia kundi hilo "liwaachilie mateka na kumaliza mzozo huo".
Matamshi hayo yalikuwa makali zaidi dhidi ya kundi hilo ambalo rais ametoa tangu vita vilipoanza miezi 18 iliyopita.
Afisa wa Hamas alilaani kile alichokiita "lugha ya dharau" ya Abbas wakati watu wake wanaelekea "…kufaidika pakubwa".
Wiki iliyopita, kundi hilo lilikataa pendekezo la Israel la kusitishwa upya kwa mapigano huko Gaza, ambalo ni pamoja na hitaji la kupokonywa silaha kwa ajili ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki sita na kuachiliwa huru kwa mateka 10 kati ya 59 waliosalia.
Hamas ilisema kuwa itawakabidhi mateka wote kwa mabadilishano ya kumaliza vita na kujiondoa kabisa kwa Israel.
🚨Subscribe YouTUBE Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.