Na Carlos Claudio, Dodoma.
Tanzania imekuwa ikijikita katika ujenzi wa taasisi za haki kupitia miradi mbalimbali ya kuimarisha mahakama kwa kuwa ni nchi ambayo inaamini katika misingi ya utawala bora wa sheria.
Hayo yamesemwa Aprili 9, 2025 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof Kitila Mkumbo katika mkutano wa wadau wa masuala ya sheria pamoja na taasisi mbalimbali za serikali huku akieleza kuwa demokrasia, haki pamoja na uhuru wa binadamu ni sehemu moja wapo ya maendeleo.
Amesema kazi ya msingi ya serikali duniani ni kusimamia shughuli za maendeleo na kutoa huduma kwa wananchi hivyo ni fursa kukutana na watu wa serikali na wasiyo wa serikali pamoja na wadau wa sheria.
“Zipo nchi nyingi zinazoamini kuwa demokrasia ni changamoto kwenye maendeleo kwaio na sisi kama nchi tupo wapi? Kwamba demokrasia na maendeleo, haku za binadamu, utawala bora na maendeleo, tupeleke huduma zote za kijamii na wananchi wapate fedha, nchi ikue kiuchumi sasa hapa demokrasia na haku za binadamu inaingia wapi?”
“Maendeleo ni kitendo chochote kinacho kuongezea uwezo wa kuchagua kufanya jambo fulani, lakini pia kinachokupa fursa ya kuongeza siku za kuishi kwasababu mwisho wa siku wote hatimaye tutafariki.” amesema Kitila
Ameongeza na kusema kuwa maendeleo ni mchakato unaomsaidia mwanadamu kuongeza siku za kuishi hivyo serikali inajivunia maendeleo ya dira ya 2025 kwa kuongeza umri wa kuishi.
Kwa upande wake Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema kupitia kikao wanatazama namna gani watajenga mashirikiano ya kimkakati ili iwe chahcu ya utendaji haki na utawala bora kwa watanzania.
Aidha amewataka wadau wote wanaoshugulika na masuala ya haki, utawala wa sheria katika taifa waone umuhimu wa kufanya kazi na wadau wa sheria ikiwa wanasheria, vyama vya wanasheria, asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu na kwa ushirikiano huo utapelekea utatuzi wa tofauti zao kwa manufaa ya taifa.
“Msingi mkubwa wa majadiliano yetu ni kuwekeza zaidi nguvu katika hoja ya Mhe. Rais aliyosema mifumo yetu ya utoaji haki haisomani, sasa Rais anapozingumza inamaanisha anazungumza na nchi nzima iwamba mifumo yetu ya haki, minyororo mzima wa haki inapaswa kusomana,”
“Tumeona kwamba tuna changamoto ya kufanya kazi kwa pamoja, wakati mwengine tumekuwa tunaogopana bila sababu, tuna hisiana tofauti na zipo taasisi ambazo tumefanya kazi kwa pamoja lakini zipo ambazo pengine kutokana na viongozi ambao wapo katika taasisi hizo bado wanashindwa kutuelewa sisi kama ni wadau wakubwa sana katika mnyororo wa haki.” amesema Olengurumwa.
![]() |
🚨Full VIDEO inapatikana kwenye YouTube Channel yetu ya WASHINDI MEDIA.