Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu jioni ya leo, Alhamisi Aprili 10.2025 amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jujini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka mawili (2) tofauti ya jinai yanayosikilizwa na Mahakimu wawili (2) tofauti
Shtaka la kwanza ni la uhaini alilotenda kinyuma na kifungu cha 36, kifungu kidogo cha pili cha kanuni ya adhabu ambapo inaelezwa kuwa mnamo Aprili 03.2025 akiwa ndani ya jiji la Dar es Salaam Tundu Lissu alitoa kauli alitoa kauli inayochochea umma kuzuia uchaguzi na kutishia serikali ya Tanzania.
Akisoma shtaka hilo Mahakamani hapo Wakili Mwandamizi wa Serikali Nassor Gatuga amenukuu miongoni mwa kauli hizo kuwa ni pamoja na ile aliyosema, "Msimamo huu (wa 'No Reforms, No Election') unaashiria uasi, ni kweli kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi.., tunaenda kukinukisha"
Hata hivyo, mtuhumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwani.
Mahamakama Kuu ndio yenye mamlaka hayo, na kwa sasa Jamhuri haijakamilisha upelelezi
Shauri hilo sasa limeahirishwa hadi Aprili 24.2025 saa 5 asubuhi litakapotajwa tena Mahakamani hapo, wakati huo mtuhumiwa ataendelea 'kusota' rumande kwani shtaka linalomkabili halina dhamana.
Baada ya kukamilika kwa shtaka la awali, ndipo shtaka la pili, lenye makosa matatu (3) likasomwa Mahakamani hapo nalo ni kuchapisha taarifa za ongo YouTube Aprili 03.2025 kwa lengo la kupotosha umma.
Kosa la kwanza, imeelezwa Mahakamani hapo na Wakili Mwandamizi Serikali Nassor Gatuga kuwa mtuhumiwa alisema wagombea (wa upinzani katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024) waliengiliwa kwa maelekezo ya Rais, Kosa la pili, imeelezwa kuwa mtuhumiwa alilituhumu Jeshi la Polisi kwa kudai kuwa maafisa wake (askari) wanatumika kuiba kura wakiwa na 'vibegi', na kosa la tatu ni kupotosha umma kwa kile ambacho mtuhumiwa alieleza kuwa Majaji ni 'Ma-CCM' hawawezi kutenda haki.
Hata hivyo mtuhumiwa amekana makosa yote matatu (3) kwa kuieleza Mahakama kuwa kosa la kwanza 'siyo kweli', kosa la pili 'halijawahi kuwa kosa na siyo kweli' na kosa la tatu 'siyo kosa la jinai na siyo kweli'.